Wana 'Jihad' walimuuwa kamanda wa Hezbollah

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwili wa kamanda wa kundi la Hezbollah Mustafa Badreddine nchini Lebanon

Kundi la wapiganaji la Lebanon Hezbollah limesema kuwa Wasunni walio na itikadi kali ndio waliomuua kamanda wao mkuu nchini Syria siku ya Ijumaa,Mustafa Badreddine.

Taarifa kutoka kwa kundi hilo inasema uchunguzi umebaini kuwa bwana Badreddine aliuwawa katika shambulizi la mabomu lililotekelezwa na Wasunni walio na itikadi kali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mustafa Badreddine

Akiongea mjini Beirut, waziri wa viwanda wa Lebanon ambaye pia ni mwanachama wa Hezbollah, Hussein Haj Hassan, amesema kuwa bado wataendelea na vita.

Mustafa Badreddine amekuwa mwanachama muhimu wa oparesheni za kundi hilo akitumia majina tofauti yalio bandia kwa miongo kadhaa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hezbollah

Alituhumiwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kwa kuhusika kwa mauaji wa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri.