Paka mzee zaidi kutoka Marekani afariki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Paka mzee kutoka Marekani afariki

Paka aliyewekwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness of World record kwa kuwa mzee amefariki.

Scooter aliyesheherekea miaka 30 ya kuzaliwa mnamo mwezi Machi amefariki.

Mmiliki wake Gail Floyd kutoka Texas amesema kuwa paka huyo alifariki baada ya kuthibitishwa kuwa mzee zaidi.

Daktari Tricia Latimer,amesema kuwa Scooter aliishi kwa karibia miaka 136 ya binaadamu na amekuwa akisafiri mara kwa mara.

Kufikia sasa alikuwa ametembea majimbo 45 kati ya 50 ya Marekani.