Mashabiki 12 wa Real Madrid wauawa na IS Iraq

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgahawa wa al-Furat nchini Iraq

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wameshambulia mgahawa mmoja unaotembelewa na mashabiki wa Real Madrid na kuwaua watu 12.

Watu 3 walifyatua risasi katka mgahawa huo wa al_Furat katika mji wa Shia wa Bald nchini Iraq mapema siku ya Ijumaa.

Washambuliaji hao walitoroka na saa chache baadaye huku mmoja wao akajilipua alipokamatwa na wapiganaji wa Shia,na kuwaua wanne wao.

Baada ya kukiri kutekeleza shambulio hilo kundi la wapiganaji wa Islamic State lilisema kuwa shambulio hilo liliwalenga wapiganaji na halikuhusishwa na Real Madrid.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulio la magahawa nchini Iraq

Lakini taarifa kutoka kwa klabu ya Real Madrid ilisema kuwa mashabiki wake 16 waliuawa katika shambulio.

''Klabu hiyo ilisikitishwa sana na shambulio hilo na kutuma rambirambi kwa familia na marafiki wa waathiriwa'',ilisema taarifa.