Musumbiji yakumbwa na uhaba wa chakula

Image caption Musumbiji imeathiriwa na hali mbaya ya ukame.

Musumbiji inasema kuwa haina chakula cha kutosha kuwalisha karibu watu milioni moja walioathiriwa na ukame nchini humo.

Inasema kwa inaweza kuwalisha nusu ya watu hao. Musumbuji imeathiriwa na ukame mbaya maeneo ya kusini na kati kati mwa nchi pamoja na mvua kubwa inandamana na mafuriko.

Takriban watu 40 wameaga dunia. Maeneo makubwa yenye mimea ya kilimo yameharibiwa huku maelfu ya mifugo wakikufa.