Urusi yasema kashfa imeitia aibu

Haki miliki ya picha epa
Image caption Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko

Waziri wa Michezo wa Urusi, ameomba msamaha, kwa kashfa iliyohusu madawa ya kusisimua misuli kutumiwa kwenye michezo , kashfa ambayo inaweza kupelekea wanariadha wa Urusi kupigwa marufuku kushiriki kwenye Olimpiki nchini Brazil mwaka huu.

Katika makala yake kwenye gazeti la Uingereza, The Sunday Times, waziri huyo wa Urusi, Vitaly Mutko, alisema makosa makubwa yamefanywa, na kashfa imeitia aibu Urusi. Lakini Bwana Mutko hakusema kama serikali ilihusika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kashfa inaweza kupelekea wanariadha wa Urusi kupigwa marufuku kushiriki kwenye Olimpiki

Juma lilopita, afisa wa Urusi, wa kupambana na madawa kutumiwa kwenye michezo, Grigoriy Rodchenkov, alisema kuwa kulikuwa na mpango wa kufanya udanganyifu katika Olimpiki za majira ya baridi, zilizofanywa Sochi, miaka miwili iliyopita, na kwamba serikali iliunga mkono mpango huo.