Besigye ahamishiwa gereza la Kampala

Image caption Video imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Besigye akijiapisha kuwa rais.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anahamishwa kutoka gereza la Moroto Kaskazini Mashariki mwa nchi kwenda gereza la Luzira lililo mji mkuu Kampala ambalo ndilo gereza kubwa zaidi nchini humo.

Msemaji wa Idara ya magereza nchini Uganda Frank Baines amethitisha kuwa bwana Besigye kwa sasa yuko njiani kwenda Kampala.

Siku ya Ijumaa alishtakiwa kwa uhaini na kupelekwa rumande huko Moroto baada ya kukamatwa mjini Kampala.

Video moja imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Besigye akijiapisha kuwa rais.