Tani 8 za cocaine zapatikana Colombia

Image caption Madawa hayo yalikuwa yamefichwa kwenye shamba la ndizi .

Polisi nchini Colombia wanasema kuwa wamepata kiwango kikubwa zaidi cha madawa ya kulevya kuwai kupatikana nchini humo cha karibu na tani nane za Cocaine.

Madawa hayo yalikuwa yamefichwa kwenye shamba moja la ndizi karibu na mji ulio kaskanizi magharibi wa Turbo.

Rais Juan Manuel Santos aliwapongeza mafisa kupitia kwa mtandao wa Twitter akisema oparesheni hiyo imepata kiwango kikubwa zaidi cha madawa katika historia ya nchi hiyo.

Polisi wanasema kuwa madawa hayo ni ya kundi linalofahamika kama Clan Usuga. Washukiwa watatu walikamatwa na wengine watatu wakafanikiwa kutoroka.

Mapema mwezi huu serikali ya Colombia ilisema kuwa itaendesha mashambulizi ya angani dhidi ya makundi ya walanguzi wa madawa ya kulevya.