Watoto marufuku kushiriki vita:Colombia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mpiganaji mtoto wa kundi la FARC akiwa ameshikiliwa mateka

Serikali ya Colombia inataka kuondolewa katika jeshi la waasi wa FARC watoto wote waliochini ya umri wa miaka 15.

Uamuzi huo uliofikiwa katika mazungumzo ya amani ya Havana ni kufuatia kundi la waasi la FARC kusajili vijana walio chini ya umri wa miaka 15 na kuwa wapiganaji wa kundi hilo.

Kwa maafikiano hayo sasa watoto hao watachukuliwa kama wahanga wa vita na watapewa msamaha na serikali ya Colombia,na pia watoto hawa watarejeshwa kuungana na familia zao.

Kundi la waasi la FARC limeafiki kusaidia kuwabaini wapiganaji watoto na kuandaa namna ya kuwatoa mafichoni waliko wapiganaji wake.

Makubaliano hayo pia yanatarajiwa kuwahusisha wapiganaji watoto wenye umri wa miaka chini ya miaka 18 pia katika makundi mengine ya wapiganaji.