Libya kupewa silaha kupambana na IS

Image caption Viongozi wakijumuika katika mazungumzo ya Libya

Nchi 25 ikiwemo Marekani zimekubaliana kuipa silaha serikali ya Libya kwa lengo la kuiwezesha kukabiliana na wanamgambo wa IS wanaoendelea kuisumbua nchi hiyo.

Muungano wa kimataifa umesema kuwa utalegeza vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa juu ya Libya kutoa silaha kwa vikosi vinavyounga mkono serikali mpya ya Tripoli.

Waziri mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj, amesema kuwa IS wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwa nchi yake na msaada huo wa kimataifa utakuwa muhimu katika kupambana na ugaidi kwa mafanikio.

Nchi hizo tano ambazo ni wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa walifikia makubaliano hayo baada ya mazungumzo mjini Vienna.Libya imekumbwa na machafuko tokea kuangushwa kwa kanali Gaddafi mwaka 2011.