Mazungumzo kuhusu Libya yaanza Austria

Image caption Mawaziri wanaokutana Austria

Mawaziri wa mashuri ya nchi za kigeni kutoka Marekani, Mashariki ya Kati na Ulaya wanazungumzia mzozo nchini Libya kwenye mkutano unaofanyika katika mji mkuu wa Austria Vienna.

Wana matumaini ya kuleta utulivu zaidi nchini humo na kuiunga mkono serikali mpya.

Lakini matarajio yao ni madogo kwa sababu wanasiasa nchini Libya na viongozi wa wanamgambo wamekataa kujiunga kwa pande mbili hasimu.

Akiongea kabla ya mazungumzo hayo waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Ujerumani Frank Walter Steinmeier, alisema kuwa kuna wasiwasi kuhusu ikiwa mazungumzo hayo yatasababisha Libya kutoka hali iliyo ambayo ni ngome ya islamic state kwenda kwa nchi yenye umoja.