Savio watwaa ubingwa mpira wa vikapu Tanzania

Savio
Image caption Ni mara ya tano kwa Savio kuchukua ubingwa Tanzania

Klabu ya mpira wa vikapu ya Savio ya Upanga, Don Bosco jijini Dar es salaam imechukua ubingwa wa taifa.

Hii ni baada ya kuifunga timu ya jeshi ABC vikapu 77 kwa 66 kwenye fainali iliyofanyika jumapili ya tarehe 15 ndani ya uwanja wa taifa wa mpira wa vikapu.

Amini Mntambo wa Savio mwenye jezi namba 14 ndiye mchezaji bora wa ligi.

Michuano hiyo ilianza tarehe 7 Mei 2016 na jana jumapili ndiyo ilikuwa ni kilele chake.

Savio kwa mara ya kwanza walishiriki mashindano haya yaliyofanyika Tanga mwaka 2005 ambapo fainali walikutana na timu ya jeshi ya JKT na kuwafunga.

Savio kupitia ligi hii ya taifa wameshachukua ubingwa huu zaidi ya mara 5.

Walichukua ubingwa miaka mitatu mfululizo mwaka 2009/2010, 2010/2011, 2011/2012.

Sasa wamefuzu kucheza Zone 5 na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Upande wa kina dada, Don Bosco Lioness wa Upanga, Don Bosco jijini Dar es Salaam wamechukua ubingwa wa taifa kwa kuifunga timu ya JKT vikapu 63-62 kwenye fainali.

Oryn Londo wa Lioness mwenye Jezi namba 7 Mgongoni ndiye mchezaji bora katika mchezo wa fainali.