Kikosi cha pamoja chashambulia al-Shabab

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanamgambo wa al-Shabab

Kikosi cha pamoja cha Marekani na Muungano wa Afrika kimeendesha mashambulizi dhidi ya kambi za al-Shabab kwenye mji ulio kusini wa Somalia wa Barire ulio umbali wa takriban kilomita 60 kutoka mji mkuu Mogadishu.

Milipuko mikubwa ilisikika pamja na sauti za risasi wakati wa oparesheni hiyo dhidi ya wanamgambo hao wenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.

Wenyeji walisema kuwa vikosi vya Marekani vilitoa msaada kwa makomando wa somalia waliopewa mafunzo na Marekani na kusaidiwa na vikosi vya Muungano wa Afrika wakati viliingia mji wa Barire.

Haki miliki ya picha AP
Image caption al-Shabab wana uhusiano na al-Qaeda

Risasi zilifyatuliwa kutoka kwa helkopta za Marekani zilizokuwa angani wakati wa oparesheni hiyo.

Walisema kuwa wapiganaji wa al-Shabab walikimbia mji wa Barire wakati vikosi vya muunagno viliingia na vikosi hivyo vikaondoka baada ya kuharibu kambi za al shabab.

Hata hivyo al-Shabab wanasema kuwa wapiganaji wake walikabiliana na oparesheni hiyo.

Marekani halijazungumzia operesheni hiyo lakini maafisa wa Somalia wamethibitisha operesheni hiyo ya pamoja.