Nyumba zaendelea kubomolewa Nairobi

Image caption Ubomoaji waendelea Nairobi

Utawala nchini Kenya umerejelea shughuli ya kubomoa zaidi ya majengo 200 katika mji mkuu Nairobi ambayo yametajwa kuwa yasiyo salama kwa watu kuishi.

Utawala ulianza kuchukua hatua hiyo baada ya jengo moja la ghorofa sita, ambalo lilikuwa linatajwa kuwa lisilo salama kuporomoka na kuwaua zaidi ya watu 50 mjini Nairobi wiki tatu zilizopita.

Image caption Wakaazi wakihama kutoka kwa nyumba zinazobolewa.