Nigeria yatupilia mbali mswada wenye utata

Image caption Mswada huo ulipendekeza kifungo cha miaka saba jela au faini ya dola 25,000.

Bunge la senate nchini Nigeria limetupilia mbali mswada ulionuia kudhibiti mitandao ya kijamii ambao wakosoaji walidai ulilenga kukandamiza uhuru wa kusema.

Mwezi Disemba mwaka uliopita mswada huo ulikoselewa vikali kwa kunuia kumuadhibu yeyote ambaye ataeneza habari za uongo kwenye vyombo vya habari.

Ulipendekeza kifungo cha miaka saba jela au faini ya dola 25,000 kwa yeyote ambaye angepatika akituma ujumbe wa matusi.