Twitter kutohesabu picha na viunganishi katika ujumbe

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Twitter

Mtandao wa Twitter utawacha kuhesabu picha na viunganishi katika herufi 140 zinazohesabiwa katika ujumbe kulingana na ripoti za Bloomberg.

Mabadiliko hayo huenda yakafanyika katika kipindi cha wiki mbili zijazo ,Bloomberg imenukuliwa ikisema.

Kampuni hiyo haijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo.Lakini mnamo mwezi Januari mwanzilishi Jack Dorsey alisema kuwa twitter itatafuta njia ya kuwawezesha wateja wake kuandika ujumbe mrefu.

Viunganishi huchukua takriban herufi 23 katika ujumbe,hivyobasi kupunguza nafasi iliopo kwa wateja wakati wanapoandika ujumbe wao ili kusambaza mtandaoni.

Kiwango cha herufi 140 kinachohitajika kiliongezwa ili kuufanya ujumbe kutoshea .

Wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo mwaka 2006,kabla ya simu za smartphone kuzinduliwa wateja wengi walichapisha ujumbe wao kabla ya kuchapisha.