Dola milioni 110 zahitajika kusaidia nchi za Afrika

Image caption Ukame umesababisha ukosefu wa chakula kwenye nchi za kusini mwa Afrika

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na chama cha msalaba mwekund wametoa ombi la dola milioni 110 kusaidia nchini za kusini mwa Afrika zilizoathirika na ukame.

Takriban watu milioni 31.6 katika eneo hilo hawana chakula cha kuwatosha kutokana na ukosefu wa mvua na uhaba wa maji.

Ombi hilo linatolewa kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa umoja waimataifa, unatarajiwa kuangazia hitaji la kuchukua hatua, kulinda jamii kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.