Utata wazuka kuhusu msichana wa Chibok

Image caption Kuna utata kuhusu ni nani alimuokoa na jina la msichana ni lipi.

Kumezuka utata kuhusu msichana wa Chibok ambaye aliokolewa nchini Nigeria. Kwanza jeshi linasema kuwa ndilo lilimuokoa msichana huyo aliyetjwa jina kuwa Falmata Mbalala.

Hata hivyo wanaharakati na viongozi wa kijamii wanasema kuwa msichana aliyeokolewa, jina lake ni Amina Ali Nkek na kuwa alipatikana katika msitu wa Sambisa na kundi la vijana na kudumisha usalama.

Msitu huo ndio maficho makuu ya wanamgambo wa Boko Haram.

Mwenyeki wa chama cha wazazi wa Cibok mjini Abuja Hosea Abana Tsambido aliiambia BBC kuwa vijana hao walikuwa na habati kubwa kumpata msichana huyo.