Msichana wa Chibok akutanishwa na familia yake

Haki miliki ya picha AP
Image caption Amina Ali Nkek amekutanishwa na familia yake.

Msichana wa Chibok ambaye aliokolewa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram baada ya zaidi ya miaka miwili amekutanishwa kwa muda mfupi na familia yake.

Wanajeshi walimpeleka Amina Ali Nkek kwenda mji wa Mbalala karibu na Chibok, na kumrudisha tena baada ya familia yake kudhibitisha kuwa alikuwa ndiye yeye. Alikuwa na umri wa miaka 17 wakati alitekwa nyara.

Mwenyekiti wa cha chama cha wazazi wa Chibok Hosea Abana Sambido, aliambia BBC kuwa msichana huyo ametambuliwa na familia yake.