Mvua kubwa yasababisha maafa Sri Lanka

Shirika la msalaba mwekundu nchini Sri Lanka, linasema kuwa zaidi ya familia 200 hazijulikani ziliko, baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyosomba kabisa vijiji vitatu katikati mwa kisiwa hicho.

Msemaji wa shirika hilo amesema kwamba kumekuwepo na tahadhari ya mapema, na huenda baadhi ya familia ilihama, lakini idadi kamili bado haijatolewa.

Huku akizuru maeneo yaliyoathirika, Rais Maithripala Sirisena, ameiambia BBC kuwa hitaji kuu kwa sasa ni kuwapata watu hao waliotoweka na kuwahudumia mamia kwa maelfu ya watu waliohamishwa makwao.

Maeneo mengi ya nchi hiyo imekumbwa na mafuriko. Wakuu wanasema watu 37 wamefariki.