Rais Maduro:Marekani inataka kunipindua

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Venezuela Nicolas Maduro aishutumu Marekani kutaka kumuangusha

Rais wa Venezuela Nicolaus Maduro ameshutumu Marekani kwa madai ya kufanya njama ya kutaka kuipindua nchi yake.

Rais huyo pia ameishutumu Marekani kwa madai ya kupanda mbegu ya machafuko katika nchi hiyo.

Wakati huo huo Kiongozi wa upinzani nchi humo Henrique Capriles amelitaka jeshi la nchi hiyo kuchagua kumtii Rais Maduro au kuitii katiba akimshutumu rais huyo kwa kutangaza hali hatari wiki iliyopita.

Capriles amemshutu bwana Maduro kwa kutangaza hali ya tahadhari nchini humo wiki iliyopita. Kabla ya bunge la nchi hiyo kupinga uamuzi huo wa rais, Maduro alisema agizo hilo lilihitajika kwa sababu uhuru wa taifa hilo ulikuwa unakabiliwa na mashambulio ambayo hayakutarajiwa.