Manny Pacquiao achaguliwa kuwa Seneta

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manny Pacquiao akipambana na Floyd Mayweather.

Bondia raia wa Ufilipino Manny Pacquiao, ameshinda kiti kwenye bunge la senate la nchi hiyo.

Pacquiao ni ni kati ya masenata 12 wapya waliochaguliwa katika bunge la juu wakati wa uchaguzi wa hivi majuzi.

Alipata kura milioni 16.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wengi wanaamini ushindi utotaa fursa katika jaribio lake la kushinda urais siku za usoni.

Wengi wanaamini kuwa uchaguzi huo wa mmoja wa watu maarufu zaidi duniani katika ulingo wa ndodi, utotaa fursa katika jaribio la kushinda urais siku za usoni.

Pacquiao ameshinda mataji kadha makubwa duniani na kuwa mwakilishi wa bunge wa chini nchini Ufilipino.