Mbwa awang'ata watoto 11 Uingereza

Image caption Mbwa Uingereza

Watoto 11 wamejaruhiwa katika shambulio la mbwa katika eneo la kuchezea lililozungushiwa uwa.

Mbwa huyo wa Staffordshire alizuiliwa na mzazi mmoja baada ya kuwang'ata watoto hao huko Blyth Northumberland.

Watatu kati ya watoto hao ,ambao walikuwa na majeraha baada ya kushindwa kutoka katika eneo hilo walilazwa hospitalini usiku kucha baada ya shambulio hilo la siku ya Jumatano.

Maafisa wa polisi baadaye walimkamata mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumiliki mbwa asiyeweza kumdhibiti.

Image caption Mbwa Uingereza

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni msichana mmoja wa miaka saba ambaye anahitaji kufanyiwa upasuaji.

Baba ya mmoja wa watoto waliojeruhiwa alifanikiwa kumfunga mbwa huyo katika uwa,kabla ya maafisa wa polisi kuwasili ili kumpeleka katika kibanda chake.