Marekani yahofia uvamizi kimitandao

Haki miliki ya picha Getty
Image caption James Clapper,mkuu wa upelelezi wa Marekani

Mkurugenzi wa Upelelezi nchini Marekani, James Clapper, amesema kuna ushahidi kwamba wavamizi wa mitandao wanaofanya kazi na serikali za kigeni na wamejaribu kuwalenga wagombea katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu.

Clapper amesema maofisa wa serikali wamekuwa wakifanya kila wawezalo kuwashauri wagombea juu ya jinsi ya kuweka data zao salama.

Lakini amesema anatarajia mashambulizi zaidi kwa jinsi kampeni zinavyoendelea.Maafisa hao wameitambua China kama chanzo cha mashambulizi dhidi ya wagombea wote wa Urais kutoka Democratic na Republican katika chaguzi mbili zilizopita.Mwaka huu makundi mbalimbali ya uvamizi mitandaoni yamekuwa yakitishia kampeni za bwana Donald Trump.