Rwanda mbele Afrika Mashariki kwa umri wa kuishi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chanjo imepunguza viwango vya watoto wanaofariki

Umri wa kuishi barani Afrika unaongezeka kwa haraka ikiwa ni maradufu sawa na maeneo mengine duniani kulingana na shirika la afya dunia WHO.

Rwanda ndiyo inayoongoza Afrika Mashariki, umri wa kuishi nchini humo ukiwa miaka 66.1.

Ripoti ya WHO inasema tangu mwaka 2000, umri wa kuishi umeongezeka kwa takriban miaka 10 zaidi. Kwa sasa mtu wa wastani anaweza kuishi hadi miaka 60.

Lakini Umri huo bado ni miaka 20 chini ya mtoto anayezaliwa katika mojawapo ya mataifa 29 yenye mapato makubwa.

Daktari Ties Boerma kutoka WHO ameimbia kipindi cha Newsday cha BBC kwamba sababu moja ni kupungua kwa vifo miongoni mwa watoto inayofanywa na chanjo.

Haya hapa mataifa yenye viwango vya juu vya umri wa kuishi Afrika:

  1. Algeria - 75.6
  2. Tunisia - 75.3
  3. Mauritius - 74.6
  4. Morocco - 74.3
  5. Cape Verde - 73.3
  6. Seychelles - 73.2
  7. Libya - 72.7
  8. Misri - 70.9
  9. Sao Tome - 67.5
  10. Senegal - 66.7
Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Robert Mugabe ana umri wa miaka 92

Taifa la Ethiopia ni la 16 katika orodha hiyo likiwa na kiwango cha kuishi cha wastani wa miaka 64.8, Kenya ikiwa ya 22 na miaka 63.4,Ghana iko katika nafasi ya 25 ikiwa na miaka 62.4, Somalia ni ya 47 ikiwa na miaka 55 na Nigeria ni ya 48 ikiwa na miaka 54.5.

Umri wa kuishi katika eneo la Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara:

Algeria 75.6
Mauritius 74.6
Cabo Verde 73.3
Ushelisheli 73.2
Sao Tome na Principe 67.5
Senegal 66.7
Rwanda 66.1
Gabon 66
Namibia 65.8
Botswana 65.7
Madagascar 65.5
Ethiopia 64.8
Eritrea 64.7
Congo 64.7
Comoros 63.5
Kenya 63.4
Mauritania 63.1
Afrika Kusini 62.9
Ghana 62.4
Uganda 62.3
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 61.8
Zambia 61.8
Niger 61.8
Liberia 61.4
Gambia 61.1
Zimbabwe 60.7
Benin 60
Burkina Faso 59.9
Togo 59.9
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 59.8
Burundi 59.6
Guinea 59
Swaziland 58.9
Guinea-Bissau 58.9
Malawi 58.3
Mali 58.2
Equatorial Guinea 58.2
Msumbiji 57.6
Sudan Kusini 57.3
Cameroon 57.3
Nigeria 54.5
Lesotho 53.7
Côte d'Ivoire 53.3
Chad 53.1
Jamhuri ya Afrika ya Kati 52.5
Angola 52.4
Sierra Leone 50