Daniel Craig azidi kutafakari kuhusu James Bond

James Bond Haki miliki ya picha AP
Image caption Craig ameigiza katika filamu nne za 007

Mwigizaji mashuhuri Daniel Craig bado hajaamua iwapo ataendelea kuigiza kwenye filamu nyingine ya James Bond, ajulikanaye kama 007.

Kumekuwa na taarifa zilizodokeza kwamba mwigizaji huyo, aliyeigiza kama James Bond katika filamu nne, amekataa nafasi ya kuigiza katika filamu nyingine.

Haki miliki ya picha AFP

Lakini duru za kuaminika zimeambia BBC kwamba Craig bado hajafanya uamuzi kuhusu 007.

Aidha, huenda asifanye uamuzi huo “hivi karibuni”.

Haki miliki ya picha PA

Mapema mwaka huu, MGM, wanaomiliki haki za kibiashara za 007, waliambia wawekezaji kwamba filamu za James Bond zitakuwa zikitolewa kwa mzunguko wa miaka mitatu au minne.

Filamu ya majuzi zaidi, Spectre, ilizinduliwa mwaka 205.

Hii ina maana kwamba filamu ijayo inatarajiwa 2018 au baadaye.