Uganda yapiga marufuku uvutaji Sigara hadharani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uganda yaweka Sheria kali kupambana na uvutaji Sigara

Sheria kali dhidi ya uvutaji sigara na uuzaji wa tumbaku imeanza kufanya kazi nchini Uganda

Watu wanaowasha sigara kwenye baa,migahawa na hoteli watalipa faini ya dola 60 au kifungo cha mpaka miezi miwili.

Wavuta sigara wanapaswa kuwa umbali wa mita 50 kutoka kwenye maeneo ya hadhara, kama vile Shule,Hospitali na kwenye maeneo ya usafiri wa umma

Sheria mpya zinawabana pia wauzaji wa sigara za kilektroniki, na shisha ambazo zimekuwa maarufu sana kwenye kumbi za burudani za usiku jijini Kampala.

Zaidi ya hayo katika hatua za kupambana na uvutaji sigara, Serikali imepiga marufuku uuzwaji wa sigara moja moja na kuweka makali zaidi kwenye matangazo na uuzaji wa tumbaku kwa walio chini ya miaka 21.