Bashir
Huwezi kusikiliza tena

Uganda yashtakiwa kwa kutomkamata Bashir

Shirika moja la ubia wa mawakili nchini Uganda limeishitaki serikali ya Uganda kwa kukosa kumkamata Rais wa Sudan Omar al-Bashir alipokuwa Uganda wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni.

Hatua hiyo ya shirika la Legal Brains Trust (LBT) imejiri baada ya kutokea taarifa kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imeitaka Uganda kujieleza ni kwanini haikumkamata Bw Bashir anayetafutwa na mahakama hiyo.

Mwandishi wa BBC aliye Kampala Siraj kalyango na maelezo zaidi.