Picha za mabaki ya EgyptAir zatolewa

Jeshi la misri limetoa picha za vifaa vilivyopatatikana wakati wa shughuli ya kutafuta ndege iliyopotea ya EgyptAir katika bahari ya Mediterranean.

Kati ya picha zilizowekwa ni pamoja na jaketi za kuokoa maisha, sehemu za viti, na vifaa vingine vyenye nembo ya EgyptAir.

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea mjini Paris nchini Ufaransa ikiwa na watu 66, wakati ilitoweka kutoka kwa mitambo ya radar siku ya Alhamisi.

Wachunguzi nchini Ufaransa wamethibitisha ripoti kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe kuwa moshi ulikuwa kwenye ndege muda mfupi kabla itoweke.

Lakini hata hivyo wanasema kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege bado hakijulikani.

Shughuli hiyo ya kutafuta pia imepata sememu za wanadamu na mizigo.

Sehemu kubwa ya ndege hiyo na visanduku viwili vya kunasa mawasiliano ya ndege havijapatikana.