Maporomoko ya ardhi yawaua zaidi ya watu 70 Sri Lanka

Image caption Mafuriko nchini Sri Lanka.

Utawala nchini Sri Lanka unasema kuwa zaidi ya watu 70 sasa wanafahamika kuaga dunia kwenye maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Zaidi ya watu wengine 120 bado hawajulikani waliko.

Katika maeneo mengine ya mji mkuu Colombo, maji yalipungua kwa kiasi leo Jumamosi lakini kwenye sehemu zingine maelfu ya watu waliolazimika kuhama kutokna na mafuriko na maporomoko ya Udongo bado wanaishi kwenye makao ya muda.

Misaada ya dharura yakiwemo mahema na mashua sasa vinawazili kutoka nchini India.