Magufuli amfuta kazi waziri kwa kuwa mlevi

Image caption Yaripotiwa kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tznania Charles Kitwanga amefutwakazi kutokana na sababu ya kuwa mlevi akiwa kazini.

Kwenye taarifa, rais John Magufuli alisema kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.

Hata hivyo bwana Kitwanga hajasema lolote.

Haki miliki ya picha Statehouse Tanzania
Image caption Rais John Magufuli

Rais Magufuli ambaye aliingia ofisini mwaka uliopita aliahidi kupambana na ufisadi na awewafuta kazi maafisa kadha kuhusiana na suala la ufisadi.

Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa kufutwa kwa bwana Kitwanga ni jambo la kushangaza kwa sababu amekuwa rafiki wa rais kwa siku nyingi.