Uchunguzi wa ajali ya EgyptAir utachukua muda

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ndege hiyo iliwauwa abiri wote 66 waliokuwemo.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, anasema kuwa kila kitu kinachoaminiwa kusababisa ajali, kinasalia jinsi kilivyo kuhusiana na ajali ya ndege ya EgyptAir, iliyoanguka siku ya Alhamisi.

Bwana Al-Sisi amesema pia kuwa uchunguzi utachukua muda mrefu kukamilika huku akiviomba vyombo vya habari kujiepusha kueneza uvumi kuhusiana na kiini cha ajali hiyo.

Haki miliki ya picha EGYPTIAN ARMED FORCES
Image caption Baadhi ya mabaki ya ndege yaliyotolewa baharini

Ndege hiyo iliwauwa abiri wote 66 waliokuwemo.

Hapo jana Jumamosi, wachunguzi wa Misri walisema ni mapema mno kufikia hatma ya kilichosababisha ajali hiyo kwani uchunguzi wa data bado haujakamilika.

Kikosi kinachoendelea na msako kinaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo pamoja na kisanduku cha kuhifadhi mawasiliano ya ndege.