Waziri mkuu wa India aitembelea Iran

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amewasili nchini Iran, ikiwa ni ziara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, baada ya kumalizika kwa vikwazo ilivyoekewa Iran.

Mazungumzo na Rais Hassan Rouhani yanatarajiwa kuangazia mipango ya kuendeleza bandari ya kusini mwa Iran, Chabahar.

India imewekeza katika mradi huo, ambao utawezesha biashara kati ya India, Iran na Afghanistan kwa kupitia Pakistan.

Shirika la habari la Iran -IRNA- limesema Rais wa Afghan Ashraf Ghani ataitembelea pia nchi hiyo leo Jumatatu kusaini makubaliano hayo ya utatu.