Watu watakiwa kutumia maji kwa uangalifu India

Image caption Waziri mkuu wa India Narendra Modi

Waziri mkuu wa India Narendra Modi, ametoa wito kwa watu kutumia maji kwa uangalifu wakati nchi hiyo inakumbwa na ukame mbaya.

Akizungumza kupitia ujumbe uliotangazwa na raidio ya taifa , bwana Modi alisema kuwa maji ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.

Watu kadha wameaga dunia nchini India kutokana na joto kali. Siku mbili zilizopita India iliandikisha viwango vya juu zaidi vya joto katika historia yake.