Volkeno yaua watu 7 nchini Indonesia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majivu imerushwa angani huku tope la volkeno likitapakaa kilomita

Idadi ya watu waliofariki kufikia sasa Nchini Indonesia imepata na kufikia saba.

Watu hao wamefariki na wengine kadhaa kupata majeraha mabaya baada ya kuchomwa na gesi iliyochangamana na moshi wa volkeno baada ya mlima mmoja kulipuka magharibi mwa nchi hiyo.

Habari zaidi zinasema kuwa majivu imerushwa angani huku tope la volkeno likitapakaa kilomita tatu na kusababisha vifo vya watu hao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu waliovunikwa na majivu ya volkeno

Waathiriwa wote waliofariki walikuwa shambani wakilima katika eneo ambalo lilitangazwa na wakuu wa Indonesia kama maeneo hatari kwa kuwa karibu mno na mlima wa volkeno wa Sinabung.

Makundi ya uokoaji yamefika maeneo hayo ili kuwahamisha watu na kutafuta manusura au maiti zaidi ya waliofariki.