Kerry afanya ziara nchini Myanmar

Haki miliki ya picha
Image caption Ziara ya Kerry ni ya kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia na kiuchumi nchini Myanmar.

Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, anazuru Myanmar.

Hiyo ni ziara ya kwanza kabisa tangu utawala mpya wa kidemokrasia kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha zaidi ya nusu karne.

Katika mkutano na Bi Aung San Suu Kyi, Bwana Kerry amesema kuwa, kwa Myanmar kuingia katika mkondo wa demokrasia baada ya miaka mingi ya utawala wa kijeshi, ni hatua kubwa iliyosifiwa na wengi duniani.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekania inasema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia na kiuchumi nchini humo.