Binali Yildirim achaguliwa kiongozi wa AK Uturuki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Binali Yildirim

Binali Yildirim amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala nchini Uturuki cha AK, katika kile kinachoonekana kama hatua nyingine ya Rais Recep Tayyip Erdogan, kuongeza madaraka yake.

Kuchaguliwa kwake ni baada ya waziri mkuu wa zamani, Ahmet Davutoglu kulazimika kuondoka, baada ya kukataa mpango wa Rais Erdorgan, kuzidisha madaraka ya rais.

Awali bwana Yildrim ambaye anatajwa kuwa mfuasi wa karibu wa Erdogan alikiambia chama kuwa atafanya kazi kwa karibu na rais.

Mtangulizi wake, Ahmet Davutoglu, alikuwa na mzozo na rais ikiwemo mipango yake ya kuongeza mamlaka ya rais.