Ghasia zazidi mashariki mwa Ukraine

Haki miliki ya picha AP

Wakuu wa jeshi wa Ukraine, wanasema kuwa ghasia zimezidi mashariki mwa nchi.

Wanasema kuwa wapiganaqji wanaopendelea Urusi, wamevunja makubaliano ya kusitisha mapigano, mara 30, katika saa 24 zilizopita, pamoja na matumizi ya mizinga ambayo imepigwa marufuku katika mkataba wa Minsk.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wafungwa wa vita nchini Ukrain

Inaarifiwa kuwa mabomba ya maji yaliyoharibika, yamekata huduma kwa miji kama Luhansk, na wapiganaji wamekataa mabomba hayo kutengenezwa.

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Stepan Poltorak anasema Urusi inazidisha wanajeshi wake mpakani.