Utafiti: Uislamu hauingiani na maadili ya UK

Image caption Waislamu nchini Uingereza

Idadi kubwa ya Waingereza wanaamini Uislam hauingiliani na maadili ya Uingereza,kura moja ya maoni imesema.

Utafiti ho pia ulibaini kwamba thuluthi moja ya wale waliohojiwa wanaamini Islam ni dini inayopenda fujo na hukuza ghasia nchini Uingereza.

Hatahivyo utafiti huo pia umebaini kwamba vijana wanauelewa sana Uislamu ukilinganisha na wazee.

Zaidi ya Waingereza 2000 walihojiwa katika mtandao na kampuni ya ComRes kwa kundi la vijana la wahisani la Hamadiya Muslim Youth.

Walipoulizwa iwapo Uislamu unakuza amani nchini Uingereza,asilimia 42 ya watu wazima kati ya miaka 18 hadi 24 walikubali ikilinganishwa na asilimia 30 ya watu wazima walio juu ya umri wa miaka 25.

Image caption Kijana anayesoma Quran

Waliopulizwa iwapo wanakubaliana kwamba Uislamu unaingiliana na maadili ya Uingereza,asilimia 43 ya watu wenye umri wa miaka 18 hadi 24 walikubaliana huku makundi mengine yakipata asilimia 31.

Farhad Ahmad mwenye umri wa miaka 24 ni Imam na mwanachama wa kundi la kiislamu la Ahmadiyya.Alisema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo.

''Nadhani matokeo hayo yanatokana na ujinga.Najua hakuna mafundisho ya kiislamu ambayo yanamzuia mtu yeyote kuingiliana na jamii.Uislam unafunza utiifu kwa taifa lako''.