Milipuko mikubwa yakumba ngome za rais Assad

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Assad

Takriban watu 65 wamefariki katika milipuko ya mabomu kadhaa katika maeneo muhimu ya pwani yanayodhibitiwa na serikali ya Syria ,ripoti zinasema.

Milipuko ilikumba miji ya Tartus na Jableh.

Milipuko kadhaa ilisababishwa na walipuaji wa kujitolea muhanga,kundi moja la uchunguzi limesema.

Vyombo vya habari vya Syria vinasema kuwa vituo vya mabasi ni miongoni mwa maeneo yaliolengwa .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ngome za Assad zalipuliwa

Hospitali moja pia inadaiwa kushambuliwa.

Mashambulio kama hayo si kawaida katika eneo hilo.Hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza milipuko hiyo.