Eritrea yasherehekea miaka 25 ya uhuru

Image caption Watu wengi kutoka Eritrea huomba kupewa hifadhi katika nchi za ulaya kuliko nchi yoyote ile ya bara la Afrika.

Eritrea inasherehekea miaka 25 ya uhuru wake kutoka Ethiopia.

Shere hizo zinafanyika katika mitaa ya mji mkuu Asmara kwa bendi za muziki, wacheza ngoma na wasanii waliovalia kama wanajeshi waasi waliopigana vita vya miaka 30 ya uhuru.

Watu wengi zaidi kutoka Eritrea huomba hifadhi katika nchi za ulaya kuliko nchi yoyote ile ya bara la Afrika, na inakosolewa pakubwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Lakini hata hivyo maelfu ya raia wa nchi hiyo wanaoishi nchi za kigeni wamerudi nyumbani kujiunga na serikali.