Ugiriki kupunguziwa madeni

Baada ya mazungumzo marefu ya usiku mjini Brussels, mawaziri hao pia wamekubaliana kuingiza utaratibu wa kusamehe madeni katika kipindi cha miaka miwili -- sharti kubwa kwa Athen na shirika la Fedha Duniani.

Jopo hilo la mawaziri kumi na tisa limesema makubaliano hayo yamewezekana kuwa rahisi kutokana na jitihada za Ugiriki za kufanya mabadiliko ya kiuchumi.

Mkuu wa viongozi hao wa Jumuia ya Ulaya, Jeroen Dijselbloem ameitaja hatua hiyo kuwa ni kubwa zaidi.

IMF imeipokea kwa mikono miwili hatua hiyo ya kutambua kuwa hali ya mdororo wa kiuchumi imepitiliza hivyo utaratibu wa kusamehe madeni unahitajika.