Maporomoko ya ardhi yawazika watu kadha Myanmar

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Migodi ya jade

Ripoti kutoka kaskazini mwa Myanmar zinasema kuwa watu kadha wanahofiwa kuzikwa nchini ya maporomoko ya udongo katika eneo moja la vijijini.

Afisa mmoja katika jimbo la Kachin anasema kuwa takriban maiti kumi na moja zimeondolewa kutoka vifusi kwenye mgodi wa Hpakant.

Maporomo mawili ya ardhi katika migodi ya jade iliwaua zaidi ya watu 100 mwaka uliopita.

Migodi ya jane hutoa kiwango kikubwa cha mawe ambayo watu nchini Burma huenda kutafuta mawe yenye thamani.