Bintiye Tutu aacha kazi kwa kufunga ndoa na mwanamke

Haki miliki ya picha AP
Image caption Askofu mtaafu wa kianglikana Desmond Tutu

Bintiye askofu mstaafu wa kanisa la kianglikana Afrika kusini, Desmond Tutu, ameshurutishwa kuacha kazi yake ya ukasisi wa kanisa la kianglikana baada ya kufunga ndoa na mwanamke kinyume na sheria za kanisa hilo.

Mpho Tutu-van Furth sasa amevuliwa madaraka ya kuongoza ibada zote za kidini kwani kanisa hilo linapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini linapinga vikali ndoa za wapenzi wa jinsia moja, japo ndoa hizo zilihalalishwa nchini humo miaka 10 ilopita.

Baada ya binti wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini humo desmond Tutu, kumwoa mwanamke mwenzake, ilibidi avuliwe majukumu yake kama kasisi.

Kwa sasa Mpho Tutu-van Furth hatohusika na majukumu yake ya hapo awali ya kidini yakiwemo, kuongoza ibada za mazishi, kuongoza sakramenti takatifu na pia hataongoza sherehe za harusi.

Image caption Mpho Tutu-van Furth hatohusika na majukumu yake ya hapo awali ya kidini.

Bi Tutu amesema haya akiongea na shirika la habari la AP hivi leo.

Babake mzazi , Askofu mstaafu Desmond tutu alihuzunishwa sana na taarifa hiyo, japo hakushtuka saana.

Bi tutu anakiri wazi kuwa sheria za kanisa la kianglikana nchini Afrika kusini zinaelezea wazi kuwa ndoa ni kati ya mwanamke na mwanamme.

Anasema baada ya kufunga ndoa, askofu wa kanisa la Saldanha Bay alishauriwa kufuta leseni yake, lakini Bi tutu aliamua kuirejesha yeye mwenyewe kabla ya kunyang'anywa.

Wachumba hao wapya, Mpho na Marceline Tutu-van Furth wamekuwa fungate katika kisiwa cha Indonesia cha Bali.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tutu ana umri wa miaka 84 na afya yake sio nzuri

Kila mmoja ana watoto, kutoka kwa ndoa ya awali.

Desmond tutu ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 84, afya yake imedhoofika, lakini hilo halikumfungia kuhudhuria harusi ya bintiye mapema mwezi huu.

Bwana tutu amewahi kuskika akiunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja.