UN yaitaka Kenya iheshimu haki ya kuandamana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umoja wa mataifa waitaka Kenya kuheshimu haki ya kuandamana.

Shirika la haki za binadamu la umoja wa mataifa limesema kwa lina wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa ghasia kwenye maandamano ya kila wiki nchini Kenya.

Polisi nchini Kenya walinukuliwa na shirika la habari la AFP wakisema kuwa kuwa, watu watatu waliuawa wakati waaandamanaji walikabiliana na polisi sehemu tofauti za nchi siku ya Jumatatu.

Image caption Polisi wa kuzima maandamano

Kwenye taarifa UNHCR ilitoa wito kwa serikali kuheshimu haki ya kukusanyika kwa amani, na pia kuwa kuwataka waandamanaji kuwa na amani.

Ndiyo wiki ya nnne ya maandamano yaliyoitishwa na upinzani kutaka kuvunjwa kwa tume ya uchaguzi nchini humo.