Kingo za mto Arno zaporomoka Italia

Sehemu ya kingo ya mto Arno katika mji wa Florence nchini Italia imeporomoka mapema leo na kusababisha magari yaliyokuwa yameegeshwa eneo hilo kutumbukia kwenye shimo lililoibuka .

Kisa hicho kilitokea karibu na daraja maarufu lenye urefu wa mita 200.

Wazima moto wanaamini kuwa kuboromoka huku kumesababishwa na kuharibika kwa mfereji wa maji ulio chini ya ardhi.

Meya wa mji wa Florence anasema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho.

Ametoa wito kwa wenye magari kuondoa magari yao karibu na eneo hilo na kusema kuwa huduma za maji kwenda sehemu za mji zilikatwa.