Akiri shtaka la wizi wa picha za utupu

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Muhalifu wa mtandaoni

Mtu aliyeshtakiwa kwa wizi wa picha za utupu wa watu maarufu amekiri mashtaka yanayomkabili.

Ryan Collins mwenye umri wa miaka 36 na baba kutoka eneo la Pennsylvania ,amekiri kuiba picha hizo miaka miwli iliopita.

Alitumia mbinu ya kuhadaa na kupata nywila za watu hao kabla ya kuingia katika akaunti zao za icloud na Gmail.

Hakuna ushahidi kwamba alichapisha picha hizo katika mtandao,lakini viongozi wa mashtaka wanataka ahudumie kifungo cha miezi 18 jela.

Wizi huo wa picha mnamo mwezi septemba mwaka 2014 ulizilenga akaunti 50 za Apple na akaunti 72 za Gmail kulingana na gazeti la Los Angels Times.

Jennifer Lawrence, Kaley Cuoco na Kirsten Dunst ni miongoni mwa watu maarufu waliolengwa.