Wanariadha 14 wa Urusi na hatia ya kutumia dawa

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Wanariadha 14 wa Urusi walioshiriki mashindano ya olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing, walipatikana na hatia ya kutumia dawa zinazosisimua misuli.

Kamati ya Olimpiki nchini Urusi imesema kuwa wanariadha wake 14 walioshiriki mashindano ya olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing, walipatikana na hatia ya kutumia dawa zinazosisimua misuli wakati sampuli zao zilifanyiwa uchunguzi.

Waziri wa michezo nchini Urusi Vitaly Mutko, alisema kuwa habari kuhusu matokeo hayo hazionyeshi picha nzuri,.

Lakini akiongea na mhariri wa michezo wa BBC mjini Moscow, bwana Mutko, alisema kuwa matokeo hayo hayaashirii picha kamili na halisi ya matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu za mwili nchini Urusi.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Vitaly Mutko anasema matokeo hayo hayaashirii picha kamili na halisi ya matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu za mwili nchini Urusi.

Kwa sasa wanariadha wa nchi hiyo wamepigwa marufuku katika mashindano ya kimataifa.

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC) ilisema mapema kuwa hadi wanariadha 31 watapigwa marufuku ya kushiriki mashindano ya Rio.

(IOC) ilisema ilichukua uamuzi huo mgumu ila kuhakikisha kuwa wanariadha walio wasafi watashiriki mashindano ambayo yatafanyika kati ya tarehe 5 hadi 12 mwezi Agosti.

Aidha amesema kuwa chama cha kimataifa cha wanariadha kinalaumiwa kwa kuwaficha wanariadha waliokuwa wakitumia madawa hayo na jukumu lao sio kuwaadhibu.