Waliobadili jinsia kutumia vyoo watakavyo

Haki miliki ya picha Getty

Majimbo kumi na moja ya Marekani yanaushtaki utawala wa Rais Barack Obama, dhidi ya agizo lake kwamba shule za umma lazima wanafunzi waliobadili jinsia kuchagua vyoo vya kutumia.

Utawala huo umetishia kutotoa fedha za shirikisho kwa shule ambazo hazitazingatia agizo hilo, lakini madai hayo yaliyofunguliwa mjini Texas serikali imesema kwamba inajaribu kuzirejesha Shule katika maabara kwa ajili ya majaribio makubwa ya kijamii.

Utata umelenga katika jimbo la North Carolina,ambalo siku za hivi karibuni lilipitisha sheria likiwaruhusu watu waliobadili jinsi zao kutumia maliwato za umma kulingana na jinsi zinavyoonesha katika vyeti vyao vya kuzaliwa.