Maandamano DRC
Huwezi kusikiliza tena

Watu 4 wafariki kwenye maandamano DRC

Polisi nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo waliwatawanya waandamanaji waliokuwa wakishiriki kwenye maandamano yaliyoitishwa na vyama vya upinzani, asasi za kutetea haki za kibinadam pamoja na demokrasia Mjini Goma na Bukavu.Waandamanaji wana dai kupinga uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph Kabila atasalia madarakani baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa mwaka huu na pia kulaani mauaji katika wilaya ya Beni.Taarifa za hivu punde za sema watu wanne wamefariki dunia mjini Goma ikiwemo askari polisi wa wawili.Mwandishi ww BBC, mashariki mwa kongo BYOBE MALENGA alitutumia taarifa ifuatayo.