Iraq yajipanga kuikomboa Fallujah

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Fallujah Iraq

Raia wachache waliofanikiwa kunasuka katika eneo la mji wa Iraq wa Fallujah wameelezea hali ilivyo eneo hilo kama mgogoro mbaya kuwahi kutokea wa kibinaadamu .

Walionaswa katika eneo hilo wanakadiriwa kuwa ni zaidi ya elfu hamsini wakati vikosi vya jeshi la serikali vinapojaribu kuukomboa mji huo ulioangukia mikononi mwa wanamgambo wa Islamic State.

Familia kadhaa zilizokumbwa na fazaa ziliambia baraza la kusimamia wakimbizi la Norway kwamba wana hofu kuwa watakufa kwa njaa endapo hawatatafuta njia ya namna ya kutoroka eneo hilo.

Msemaji wa jeshi la Iraq amesema kwamba majeshi yake yako tayari kwa awamu nyingine ya ukombozi wa mji wa Fallujah , ambayo jukumu lake kubwa ni kujihusisha katika mapambano ya moja kwa moja na kundi la wapiganaji wa IS.